HARUNA Niyonzima, amesema kuwa anamshukuru kocha mkuu wa Simba, Patrick Aussems kwa kumpa nafasi ya kuonyesha mautundu yake kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa wikiendi.
Niyonzima aliingia akitokea kusugua benchi kipindi cha pili akichukua nafasi ya Emmanuel Okwi huku matokeo yakiwa ni 1-1 hali iliyomfanya aingie akiwa na maelekezo ya mwalimu pamoja na moyo wa kujituma kutimiza majukumu yake licha ya kuwa na maumivu kwenye enka.
"Siku ya jumamosi ni siku ya historia kubwa ndani ya timu yetu, namshukuru kocha kwa kuwa na imani nami na baada ya kunipa nafasi kuingia dakika chache mbele nilipata maumivu ya enka nikasema poteleapote ni lazima nipambane kutimiza majukumu yangu.
"Lengo letu ni kuona tunafika hatua ya fainali hilo linawezekana hasa kwa namna kikosi chetu kilivyo tunaamini hatutawaangusha mashabiki wetu wa Simba ambao ni zaidi ya milioni moja pamoja na taifa langu la Rwanda," amesema Niyonzima.
Simba imetinga hatua ya robo fainali baada ya kushinda mechi tatu alizocheza Uwanja wa Taifa kwa kujikusanyia jumla ya mabao sita kwenye hatua ya makundi huku akiwa na pointi tisa kinara nni Al Ahly mwenye pointi 10.
0 COMMENTS:
Post a Comment