NI MSALA JUU YA MSALA, MAJERUHI WENGINE WAONGEZEKA SIMBA
Na George Mganga
Ni kama msala vile unataka kuwaandama Simba ambapo taarifa zilizotolewa na Daktari wa timu hiyo, Yassin Gembe zinasema wachezaji Haruna Niyonzima na beki Serges Wawa waliumia katika mchezo dhidi ya JS Saoura.
Gembe amesema wawili hao waliumia katika mechi hiyo iliyopigwa huko Bechar, Algeria kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo Simba walifungwa mabao 2-0.
Gembe ameeleza Niyonzima na Wawa wameumia enka na sababu kubwa aliyoitaja imesababishwa na nyasi bandia za uwanja wa Saoura.
"Tuna majeruhi wawili tena ambao ni Niyonzima na Wawa, wote wameumia enka 'kifundo cha mguu' lakini hali zao zinaendelea vema". Alisema.
Tayari kikosi cha Simba kimeshawasili jijini Dar es Salaam na leo kitaanza mazoezi rasmi kuelekea mechi na AS Vita Jumamosi ya wiki hii itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment