March 13, 2019


Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa Daktari wa wachezaji, Yassin Gembe, umetangaza kuwa maendeleo ya wachezaji wake, Emmanul Okwi na Erasto Nyoni kuendelea vizuri.

Gembe amesema wachezaji hao hawakusafiri na timu kuelekea Algeria kwa ajili ya mechi na JS Saoura ambayo ilimalizika kwa Simba kufungwa mabao 2-0.

Gembe amesema wawili hao watakuwa Bocco Veterani leo kwa ajili ya mazoezi na ikiwezekana wakawa sehemu ya mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita.

"Nyoni na Okwi watakuwa wanafanya mazoezi leo kwakuwa hali zao zinaendelea vema na wanaweza kuwa sehemu ya kikosi dhidi ya Vita kama Mwalimu akiwapendekeza."

Simba itaenda kucheza na Vita Jumamosi ya wiki hii kusaka tiketi ya kufuzu kuelekea hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

6 COMMENTS:

  1. Sio kama mwalimu akiwapendeka , iwe isiwe hiyo ni mechi ya kufa mtu , mwalimu atake asitake lazima awapange tena nyoni acheze beki ya kushoto . asipofanya hivyo tukifungwa asisubiri kufukuzwa , aondoke usiku huo huo . by management

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe Charahani umerogwa kabisa, unamfundisha kazi kocha? Sasa kama wewe unaweza si upewe timu tuone unavyoweza kuipanga basi... Ukweli tunawaombea mshinde, tena ikibidi mlipe yale matano ili muiwakilishe Tanzania, ila kwa nguvu hizi mnazotumia, mtamvuruga kocha halafu mpigwe tena na AS VITA kisha kocha aondoke kwao tubaki na aibu yetu Watanzania... Tutulie na tuwaombee wachezaji na benchi la ufundi afya njema ya akili, mwili na roho...Ushindi upo. Nasi Yanga tuko pamoja nanyi katika mechi hiyo, hayo mengine ya utani yanayoendelea huko mtaani potezeeni na kama kuna Mwana Yanga anayewaombea mabaya, huyo mpira haujui

      Delete
  2. Halaf timu ikiyumb mnalaum uongoz....mwache Kocha afanye kazi yake basi tusiend n matokeo mfukon japo muhim kwetu n 3 points t

    ReplyDelete
  3. KWA MECHI HIYO YA MWISHO NA KWA DHAMIRA YA KUTAKA SIMBA IINGIE HATUA YA ROBO FAINALI, LAZIMA KWENDA NA MATOKEO UWANJANI. USIPOENDA NA MATOKEO YA MFUKONI YA SIMBA KUSHINDA BASI HAKUNA SABABU YA KWENDA UWANJANI HII NI MECHI YA KUFA AU KUPONA.

    ReplyDelete
  4. Ngoja nimpangie kocha timu sababu inamshinda:
    1. Manula
    2. Coullibally
    3. Kwasi (sababu ana kasi kuliko Nyoni aliyetoka majeruhi na anakaba kuliko Tshababalala aliyesababisha krosi 2 za simba kufungwa mpk sasa)
    4. Nyoni au Wawa
    5. Juuko (uwa afukuzi mshambuliaji kwa nyuma, ana kasi na nguvu na akili na mzoefu zaidi mwchi ngumu)
    6. Kotei
    7. Chama
    8. Niyonzima (mechi zote alizoingia CAF kaweza kuiunganisha timu na kiungo mzoefu zaidi na mnyumbulifu)
    9. Kagere
    10. Boko
    11. Okwi

    ReplyDelete
  5. Kiungo mmoja mkabaji atazidiwa lazima viungo wawe wawili

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic