UONGOZI wa Simba umesema kuwa hakuna namna yoyote ya kuwazuia kupata ushindi kwenye mchezo wao wa Jumamosi mbele ya AS Vita kutokana na maandalizi ambayo yameanzwa kufanya na mikakati iliyowekwa ndani ya Simba.
Simba wanahitaji poiti tatu muhimu ili kupenya hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika kutokana na kundi D kukaa kimtego kwani kila mmoja ana nafasi ya kufuzu endapo atashinda mchezo wake wa mwisho.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wanatambua ugumu uliopo kwa wao kupata matokeo ila hakuna namna ni lazima wamchinje AS Vita kwenye Uwanja wa Taifa.
"Baada ya mchezo kuisha dhidi ya JS Saoura wachezji waliitwa na kujazwa maneno mazito na ya ushindi kuelekea mchezo wao wa mwisho dhidi ya AS Vita, hivyo wana nguvu mpya na ari mpya kitakachokwenda kutokea Jumamosi kitaushangaza ulimwengu wa soka na itatokea hilo.
"Nguvu tunayo na rekodi zinatubeba kwani tuliwashinda Al Ahly waliotunyuka 5-0 kwao sasa hawa wanatokaje kwa mfano," amesema Manara.
Simba ipo kundi D ikiwa inaburuza mkia baada ya kubaki na pointi sita ambazo ilizikusanya kwenye Uwanja wa Taifa kinara ni JS Saoura mwenye pointi nane huku Al Alhy na AS Vita wote wakiwa na pointi saba.
Sorry kaka Saleh. Nina mchango wangu wa mawazo/mtazamo juu mechi hii ya Simba vs As vita. Nomba email yako nikutumie kama utaona inafaa kusomwa na watu kupitia page yako basi uiweke hewan.
ReplyDeleteEmail yangu ni:
gervasseverine@gmail.com. Nipo tabora tz.
Upcoming sportsman.
simba nguvu moja ushindi lazima
ReplyDeleteMechi ni ngumu Ila ushindi wa 2 - 1 upo kwa Simba. Iwapo beki ya Simba itatulia na kucheza kwa umakini, tahadhari na maelewano makubwa haswa mipira ya Cross na kotoruhusu faulo karibu na goli ushindi ni dhahiri tunashinda. Kwa ni mechi hii Mabeki ndiyo watakaoamua mechi. Sina shaka magoli 2 yapo, Sina hakika kama Okwi atarejea au La. But uwepo wake ni muhimu sana ktk mechi kama hii.
ReplyDeleteyasije jirudia ya ASEC Mimosa
ReplyDelete