March 13, 2019


Tetesi mbalimbali za soka huko Ulaya zimezidi kushika na, hapa tumekuandalia zilizoteka vyombo habari Jumatano ya leo.

Chelsea inahofia kuwa haina uwezo wa kumzuia mshambuliaji wake, raia wa Ubelgiji Eden Hazard kuhamia Real Madrid.

The Blues wanatarajiwa kumuuza nyota huyo wa miaka 28 kwa angalau £100m. (ESPN)

Mchezaji mwenzake Emerson amekiri kuwa wachezaji wote wa Chelsea wanahofia kumpoteza Hazard msimu huu wa joto, lakini anaamini huenda akabadili msimamo.(Sky Sport)

Hazard amekuwa akiwindwa na Madrid kwa muda mrefu licha ya kuwa inambania mchezaji huyo ambaye ni tegemo ndani ya kikosi chao.

Kipa wa Liverpool Loris Karius ataendelea kuichezea Besiktas kwa mkopo licha ya kocha wa klabu hiyo kusema hajaridhishwa na utendakazi wa mchezaji huyo wa miaka 25. (ESPN)

Vilevile ripoti zinasema Karius huenda akaishitaki Besiktas kwa kutomlipa marupurupu yake baada ya kufanya kazi kwa miezi minne bila mshahara. (Goal)

Bayern Munich itafanya mazungumzo na mshambuliaji wa Poland, Robert Lewandowski ya kuongeza mkataba wake ambao unamalizika June 2021.

Taarifa zinasema mabingwa hao wa kihistoria nchini Ujerumani wanaweza wakamuongezea miaka mingine miwili ambao utamlazimu kuendelea kukaa na Bayern mpaka mwaka 2023. (Goal)

Manchester United inatarajiwa kumsajili winga wa Borussia Dortmund muingereza Jadon Sancho.
United ambayo inashiriki Ligi Kuu Uingereza pia imewasiliana na Barcelona kuhusiana na uwezekano wa kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Philippe Coutinho, 28. (Independent)

Wakati hayo yakijijiri, Meneja wa muda wa United, Ole Gunnar Solskjaer anajiandaa kuwapatia walinzi wake nafasi ya kujidhihirisha kuwa wanaweza kufikia matarajio yake kabla ya uamuzi kutolewa wa kumnunua beki wa kati kwa kima cha £80m msimu huu wa joto. (Sun)

Walinzi Sergio Ramos wa Uhipania na Karim Benzema wa Ufaransa walidhani kuwa Jose Mourinho angeliteuliwa kuwa meneja wa Real Madrid baada ya Santiago Solari kufutwa kazi.

Wakati wakidhani hayo, Zinedine Zidane alipewa tena nafasi hiyo siku ya Jumatatu, ikiwa ni miezi 10 baada ya kuondoka klabu hiyo. (Sport)

Gunners wamejiunga na Real Madrid, Atletico Madrid, Manchester United na Liverpool katika harakati ya kupata saini ya nyota huyo wa miaka 26. (Footy Cosmos)

Kiungo wa kati wa West Ham Declan Rice anatarajia kujiunga na timu ya taifa ya England katika mechi za kufuzu kwa kombe Euro mwaka 2020 dhidi ya Czech Republic na Montenegro. (Guardian)

Baba yake kipa wa Real Madrid, Mlinda Mlango, Thibaut Courtois amevishutumu vyombo vya habari vya Uhispania na Ubelgiji kwa kumnyanyasa mwanawe. (Independent)

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic