BAADA ya Simba kupoteza mchezo wake wa Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi mbele ya JS Saoura, sasa wachezaji wameamua kuhamishia hasira zao kwa wapinzani wao AS Vita ili kushinda na kutinga hatua ya robo fainali.
Kwa sasa kundi D limekaa kimtego kwani hakuna hata mmoja mwenye uhakika wa kutinga hatua ya robo fainali mpaka jumamosi ambapo timu zote nne zitacheza mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi.
Al Ahly ambao wana pointi saba watamenyana na JS Saoura ambao kwa sasa ni vinara wakiwa na pointi nane, huku Simba ambao wanaburuza mkia watamenyana na AS Vita ambao wapo nafasi ya tatu wakiwa na pointi saba.
Beki wa Simba mwenye miraba mnne, Pascal Wawa amesema walionyesha juhudi za kupambana kutafuta matokeo kwa manufaa ya timu pamoja na taifa ila bahati haikuwa upande wao mbele ya JS Saoura.
"Tunashukuru kwa sasa, maana tulipambana kutafuta matokeo ila bahati haikuwa yetu kwa sasa hesabu zetu ni mchezo wetu ujao dhidi ya AS Vita ambao tutakuwa nyumbani.
"Bado tuna nafasi ya kurejesha tabasamu kwa mashabiki pamoja na timu kiujumla kwani mchezo wetu mmoja upo mikononi mwetu, ushindani ni mkubwa nasi tutapambana alichopanga Mungu huwezi kupangua," amesema Wawa.
0 COMMENTS:
Post a Comment