March 18, 2019


KINDA wa timu ya Simba, Rashid Juma amesema kwa sasa kikosi kipo tayari kwa mchezo wao wa kesho dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa Uwanja wa Taifa.

Simba watamenyana na Ruvu Shooting ya Masau Bwire wakiwa na kumbukumbu ya ushindi kwenye mchezo wao wa mwisho wa ligi kuu ambao walicheza dhidi ya Stand United walishinda mabao 2 yaliyowekwa kimiani na nahodha John Bocco.

Akizungumza na Saleh Jembe, Juma amesema kuwa tayari wamekamilisha mazoezi hasa baada ya kutoka kwenye mchezo wao wa kimataifa dhidi ya AS Vita juzi.

"Tumefanya mazoezi leo asubuhi kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo wetu wa kesho dhidi ya Ruvu Shooting tutakaocheza Uwanja wa Taifa.

"Tupo tayari mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti kama ambavyo wamekuwa wakifanya kwenye michezo yetu iliyopita," amesema Juma.

Simba imecheza michezo 20 mpaka sasa ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo baada ya kujikusanyia pointi 51 kibindoni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic