BAADA ya Lipuli kubeba pointi tatu mbele ya Yanga, wachezaji wamepata muda wa kupumzika ili kupata nguvu mpya kwa ajili ya mchezo wao ujao wa kombe la Shirikisho utakaochezwa Uwanja wa Samora hivi karibuni.
Kocha wa Lipuli, Seleman Matola amesema haikuwa rahisi kwa vijana wake kupata ushindi kutokana na ushindani uliopo kwenye ligi na kasi ya wapinzani wao Yanga ilivyokuwa hali iliyomfanya awape mapumziko.
"Nimewapa mapumziko wachezaji wangu ya siku mbili, jana walikuwa nyumbani na leo pia natarajia kesho wataanza kuripoti kambini ili kuanza maandalizi ya kuitafuta Singida United.
"Kila timu imejipanga kupata ushindi nasi pia hatuna mashaka tumecheza na Singida United tunawatambua tutaendelea na kasi yetu ya ushindi mpaka kieleweke," amesema Matola.
Mshindi wa kombe la Shirikisho anapata nafasi ya kuiwakilisha nchi kimataifa, ambapo mtetezi Mtibwa Sugar aling'olewa na KMC hivyo bingwa mpya atapatikana msimu huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment