March 18, 2019


FLORENT Ibenge kocha wa AS Vita, amekiri kuwa wapinzani wao Simba walikuwa bora katika mchezo wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa Afrika hali iliyowafanya kupoteza mchezo huo.

Timu hizo zilivaana juzi Jumamosi katika mchezo huo uliojaa upinzani mkubwa kila timu ikipigia hesabu ushindi ili ifuzu hatua ya Robo Fainali ya michuano hiyo mikubwa Afrika.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, Simba ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1 kupitia kwa Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na Chama.

Ibenge amesema  walikuwa na kila sababu ya kufungwa katika mchezo huo kutokana na kiwango kikubwa kilichoonyeshwa na Simba katika kipindi cha pili cha mchezo huo.

“Simba walicheza vizuri walipunguza makosa yaliyowagharimu Congo na walijituma sana, hicho ndicho kimewafanya washinde.

“Ubora wao ulikuwa kipindi cha pili hasa katika safu yao ya kiungo na ulinzi ambayo kipindi cha kwanza iliiruhusu safu yangu ya ushambuliaji kutawala na kufanikiwa kupata bao la kwanza," amesema Ibenge.

Simba imefanikiwa kufuzu hatua hiyo baada ya kufikisha pointi tisa huku Al Ahly ya Misri ikiongoza Kundi D, wakiwa na pointi 10 baada ya kufanikiwa kuwafunga JS Saoura mabao 3-0.

2 COMMENTS:

  1. Huyu kasema kweli lakini pia angekiri kuwa juu ya kupata siri za simba kutoka kwa Zahera na mashabiki wa yanga kuwashangilia lakini bado yote hayakusaidia, ungezidi ukweli wake

    ReplyDelete
  2. Kama angekuwa kocha wa bongo basi angesema Simba ni wa kawaida, sijui refa kawabeba,sijui Simba kahonga wachezaji wetu na upuuzi mwengine mwingi nakadhalika nakadhalika.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic