March 12, 2019


Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa Ofisa Habari wake, Haji Manara, umesema utafanya mazungumzo na serikali ya kuupanua Uwanja wa Taifa uliopo Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Msemaji wake, Haji Manara, amesema itabidi wafanye hivyo ili kuwapa nafasi mashabiki wa Simba kuujaza uwanja vizuri.

Manara ameeleza hayo akisema Simba ni klabu pekee hapa Tanzania yenye mashabiki wengi zaidi hivyo ni vema kama uwanja ukitanuliwa ili kutoa nafasi kubwa ya mashabiki wa Simba kuenea.

Manara amesema watafanya mazungumzo na serikali kuona namna gani wanaweza wakasaidia suala hilo hilo akidai mashabiki wa Simba hawaenei ukiendelea kuwa na watu 60.000.

Hata hivyo Manara amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi katika mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita utakaopigwa kwenye Uwanja huo mida ya saa 1 usiku.

3 COMMENTS:

  1. Uwanja utakaojengwa makao mkuu ya nchi Dodoma wahusika wafikirie hilo la kujengwa uwanja mkubwa zaidi ya huu wa Dareslaam. Ukiachana na kashikashi za Haji Manara kwani anajua dhahiri suala la kupanuliwa uwanja wa Taifa kwa sasa sio rahisi lakini kuna kila haja ya uwanja utakaojengwa Dodoma uwe mkubwa zaidi angalau uingize watu elfu tisini 90,000 kama si laki moja 100,0000.laziam to dream big na inawezekana .

    ReplyDelete
  2. badala ya kuwaomba serikali ipanue uwanja ni vema simba ikajikita kujenga uwanja wao

    ReplyDelete
  3. Badala ya kutuambia mna mpango wa kujenga uwanja wenu wenye uwezo wa kuingiza watazamaji zaidi ya elfu sitini unaleta kejeli kwa serikali eti iongeze uwezo wa uwanja kuchukua mashabiki zaidi........Shubamiti!!!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic