Uongozi wa klabu ya Simba umetangaza viingilio vya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kati yao na AS Vita utakaopigwa Jumamosi ya wiki hii jijini Dar es Salaam
Kuelekea mechi hiyo, Manara ametaja viingilio kuwa vitakuwa ni shilingi 3000 kwa mzunguko na Orange, VIP B 10,000 na VIP A 20,000 huku Platnums itakuwa ni 100,000.
Tiketi ya Platnums itampa usafiri shabiki kwenda Uwanjani akitokea Serena Hotel mpaka Uwanjani na atakaa sehemu ambayo itaambatana na vinywaji huku akipewa na jezi.
Simba inaedna kucheza na Vita ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kufungwa maba0 2-0 na JS Saoura katika mchezo wa mwisho uliopigwa huko Bechar, Algeria.
Mbali na viingilo, Manara amewataka mashabiki Simba kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo huo kwani lengo lao kubwa ni kuhakikisha wanashinda na si kingine.
Manara ameeleza uwepo wa mashabiki na haswa wakifika 60,000 itakuwa jambo jema katika kuleta hamasa kwa wachezaji siku hiyo.
Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na wadau wa mpira hapa nchini, itapigwa majira ya saa 1 za usiku katika Uwanja wa Taifa.
ILA SIO SIRI BEKI SIMBA MNARUDISHA NYUMA SIMBA. MAKOSA YALEYALE KILA SIKU.
ReplyDeleteTatizo ni kocha Simba kwa kushindwa kuwajenga mabeki alionao kucheza kwa uwelewano. Lakini Kiufundi tatizo kubwa lipo kwenye kiungo cha Simba kwa kushindwa kutimiza makukumu yao ipasavyo na kuruhusu mashambulizi kuwaelemea mabeki peke yao.Hata hivyo waliosababisha matatizo makubwa zaidi kuhusiana na udhaifu wa Simba kwenye maeneo amabayo hawapo fiti ni viongozi wa Simba wenyewe kwani walipigiwa kelele sana kabla ya haya yote kutokea kuwa wanapaswa kuboresha backline yao kabla ya kuingia hatua ya makundi lakini wakapuuzia kabisa. Fikiria kocha kama wa Nkana fc kwa kutambua tu yakwamba Simba bado itakuwa inawakilisha eneo lake kiroho safi aliwasihi sana Simba kuisuka upya backline yao la sivyo watakutana na mambo ya aibu mbeleni lakini kwa upande wa uongozi wa Simba hakuna aliejali maoni ya wadau na sasa wanavuna pamba walizotia masikioni. Nafasi ilikuwepo ya kusajili angalau wachezaji wawili hasa wa eneo la beki na kiungo mkabaji lakini utendaji wa kazi na ulegelege wa akili unaofanya kazi kwa kasi ya mwendo wa konokono kwa baadhi ya viongozi wa Simba ni tatizo. Chukulia suala la kocha msaidizi wa Simba lilivyochukua muda kufanyiwa maamuzi? Hata watembeza bakuli wa mtaa wa jirani hawakuwahi kuwa na pengo la kocha msaidizi tangu ligi ianze. Aiza wanaziba masikio yao au wanashindwa kujiamini kufanya kazi yao kwa manufaa ya klabu viongozi wa Simba wanapaswa kujitafakari. Tunajua Mo anajitahidi vya kutosha nadhani kama hakujitokeza mwezi uliopita kuweka mambo sawa basi hali ingekuwa mbaya zaidi hivi sasa ndani ya Simba.
ReplyDelete