March 15, 2019



MLINDA Mlango namba moja wa timu ya Simba, Aishi Manula amewataka mashabiki wa wote bila kujali itikadi ikiwa ni pamoja na wale wa Yanga, KMC, Azam na timu nyingine kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Taifa kuwapa sapoti wachezaji wakiwa Uwanjani kwenye mchezo wa kimataifa.

Manula amesema kuwa uwepo wa mshabiki Uwanja wa aifa utawapa nguvu ya kupambana ili kupindua meza kibabe.

"Tunakazi kubwa ya kufanya kesho na ngumu kwa ajili ya Taifa letu, tunaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi Uwanja wa Tifa ili kutupa sapoti.

"Wachezaji tutapambana kuona tunapaa matokeo chanya mbele ya wapinzani wetu katika mchezo wetu wa kimataifa na inawezekana kwa kuwa ni tunayo," amesema Manula. 

Kwenye kundi D Simba wanaburuza mkia ila wana nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali endepo watashinda mchezo wao wa kesho mbele ya AS Vita ambao kwenye mchezo wa kwanza waliibuka na ushindi wa mabao 5-0 walipokuwa nyumbani Congo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic