March 15, 2019


KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa kesho hakuna namna yoyote ni lazima wapate ushindi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa Uwanja wa Taifa.

Simba itashuka Uwanjani majira ya saa 1:00 Usiku kucheza na AS Vita ya Congo ambayo imetia timu bongo inaendelea kuwasoma wapinzani wao mdogomdogo na jana ilifanya mazoezi viwanja  vya Gymkhana.

"Ni mchezo mgumu na tunatambua umuhimu wake hakuna jambo jingine kwetu zaidi ya kupata ushindi, ni wakati wetu kutafuta matokeo chanya na kupata nafasi ya kusonga hatua ya robo fainali," amesema Aussems.

Kwenye kundi D kwa sasa Simba inaburuza mkia ikiwa na pointi sita ambazo zote imezikusanya Uwanja wa Taifa hivyo ili kupenya kwenye hatua ya robo fainali njia ni moja tu kushinda hakuna kingine.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic