LEO Singida United majira ya saa 1:00 usiku watashuka Uwanjani kumenyana na Azam FC wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar.
Kiongozi wa Singida United Dr. Mwigulu Nchemba, amesema kuondokewa na wachezaji wengi kwenye timu yao na mabadiliko kwenye benchi la ufundi kumepelekea kushindwa kupata usawa wa kiushindani katika ligi.
"Mwaka jana Singida ilikuwa na msimu mzuri, ilimaliza katika nafasi 5 za juu kwenye ligi wachezaji wengi waliokuwepo mwaka jana mwaka huu hawapo kwa sababu mbalimbali wengine wakiwa wamepata sehemu nyingine. Sasa hivi timu imeanza kujengwa upya, sasa timu ikiwa inajengwa halafu ligi inaendelea madhara yake ndiyo ya namna hii.
"Tunachofanya sasa hivi ni kuhakikisha timu inaendelea kuwepo kwenye ligi lakini jambo lingine kule ambako tunaweza kuwa bingwa tutapambana tuwe bingwa." amesema Nchemba.
Singida United ipo nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 33 baada ya kucheza mechi 28.
We mwenyewe umegawa wachezaji yanga kwa ushabiki halafu unalalamika nn
ReplyDeleteEnter your reply...hajui atendalo asubiri kushuka daraja aukimbie uboss wa timu
Delete