March 13, 2019




LICHA ya kupoteza pointi tatu mbele ya Mtibwa Sugar mchezo uliochezwa Uwanja wa Manungu jana, Kocha wa Singida United, Dragan Popadic alishindwa kuelewana na benchi lake la ufundi mara baada ya kutaka kufanya mabadiliko dakika ya 32 kwa kumtoa mchezaji Bright Obinna ili aingie Festo Simon.

Wachezaji wa Singida United pamoja na mchezaji aliyetakiwa kutolewa (Bright Obina) kwa pamoja waligomea mabadiliko hayo hali ilioyofanya mchezo uendelee mpaka kipindi cha pili ambapo Popadic alifanikiwa kufanya mabadiliko akaingia Festo Simon.

Kocha msaidizi, Fred Minziro amekiri kwamba kuna msuguano ndani ya timu yao hasa eneo la benchi la ufundi.

"Kocha mkuu ni mgumu sana kupokea ushauri, mimi nimeingia hivi karibuni lakini nimeona kocha ni mbishi kiasi kwamba wachezaji wamekuwa wanaingilia kati kwa jinsi nilivyoona bado hali si shwari.

"Mnapokuwa mnakwaruzana kwenye benchi haileti picha nzuri na mwisho wa siku hauwezi kupata matokeo kwa style hii." amesema Minziro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic