March 3, 2019


LICHA ya Salum Aiyee kushindwa kuibeba timu yake jana mbele ya Ruvu Shooting na kupokea kichapo cha mabao 6-2 bado moto wa mshambuliaji huyo umezidi kuwaka kwani mpaka sasa anaendelea kujikita kwenye anga za kufumani nyavu.

Aiyee jana amefikisha bao lake la 14 kwenye msimamo wa wafungaji akiwaacha wapinzani wake wa karibu, Heritier Makambo wa Yanga mwenye mabao 12 pamoja na mzee wa kutetema Meddie Kagere wa Simba mwenye mabao 12.

Aiyee amesema kuwa maumivu ya kupoteza mchezo wao ni makubwa ila mpira una matokeo ya ajabu, hesabu zao ni kujipanga kwa ajili ya mchezo unaofuata.

"Ushindani ni mkubwa na kila mchezo huwa tunafikiria kubeba pointi tatu ila mambo yamekuwa magumu kwetu bado tunaendelea kupambana kutafuta matokeo ili tubaki kwenye ligi," amesema Aiyee.

Mwadui FC imecheza michezo 29 ikiwa imejikusanyia pointi 33 imeshinda michezo 9 imetoa sare michezo 6 na kupoteza michezo 14.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic