March 13, 2019


Wanachama wa klabu ya wameazimia kwa pamoja kuchukua hatua za kisheria kwa watu wanaojaribu kukwamisha harakaati za uchaguzi wa klabu hiyo ambao mpaka sasa haujafanyika kwa sababu za mvutano na shirikisho la soka nchini TFF

Mratibu wa Matawi ya Yanga mkoa wa Dar es salaam Kaisi Edwin amesema viongozi wa juu wa tasisi zinazosimamia michezo nchini wameshindwa kutatua suala hilo kutokana na kutanguliza masirahi binafsi badala ya kutenda haki.


Katika hatua nyingine Edwin amelishushia lawama shirikisho la soka Tanzania TFF kwa kile alichodai ni kuididimiza klabu hiyo baada ya kupigwa faini ya Jumla ya Tsh: million 8 kwa kukiuka kanuni za ligi kuu Tanzania bara.

Yanga imekua katika changamoto kubwa ya kiuchumi na kiuomgozi kwa muda mrefu sasa tangu kujihuzuru kwa aliyekua mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuf Manji katikati ya mwaka juzi, kutokana kukumbwa na changamoto za kiafya.

1 COMMENTS:

  1. Yanga kuweni makini na maamuzi yenu ya kuhairishahairisha uchaguzi na kutoa mianya ya kuleta sintofahamu fanyeni hiyo mikutano yenu haraka na muwasihi wanachama kuacha kukimbilia mahakamani kufungua kesi na kuleta mshikamano na umoja haraka sasa uchaguzi ufanyike mwezi 4 mkutano mkuu wa wanachama ufanyike mwisho wa mwezi 3. Ili mchakato uende haraka na muwe na uongozi unaosimamia timu kwa ufanisi....muende kwenye mfumo wa uwekezaji kuanzia mwezi 6. Fanyeni haya haraka mko nyuma sana!!!!!...leteni wawekezaji kuunda kampuni ya michezo ya Yanga kuanzia juni Mwekezaji aanze kutafutwa kuanzia mwezi 5....huo ni ushauri wangu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic