March 17, 2019



UONGOZI wa Yanga baada ya kupoteza mchezo wake wa jana kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Samora mbele ya Lipuli umesema kuwa bado kazi inaendelea kwani kukosa ushindi ni sehemu ya matokeo.

Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten amesema kuwa bado wana nafasi ya kuendelea kupata matokeo kwenye michezo inayofuata kikubwa ni mashabiki kuendelea kutoa sapoti.

"Tumepoteza mchezo hatujapoteza matumaini, bado tuna nafasi ya kuendelea kufanya vizuri na kupata matokeo chanya mashabiki mtupe sapoti," amesema Ten.

Mchezo wa jana unakuwa wa tatu kwa Yanga kupoteza baada ya kuanza kupoteza mbele ya Stand United, Simba na Lipuli na kufanya wabaki nafasi ya kwanza na pointi zao 67.

6 COMMENTS:

  1. Usiseme mashabiki kuwa mtupe sapoti lakini sema mashabiki mtupe hela na ubingwa muusahau madhali mnyama yupo hau na msijipe tamaa isiyopo. Nyie badala ya kumuomba mungu akupeni ushindi mnamuomba Mungu ainyime simba ushindi na haya ndio yanayokuharibieni

    ReplyDelete
  2. simba kwa miaka minne walikua wakishangilia timu pinzani za nje dhidi ya yanga sasa mnalazimisha yanga wawashangilie !!!

    ReplyDelete
  3. Kama kweli Simba kwa miaka minne walikuwa wakishangilia timu pinzani za nje dhidi ya Yanga basi timu ya wananchi Yanga wakati huu ilikuwa iwape fundisho wanazi wa Simba jinsi yakuwa wazalendo kwa watu wa Yanga kuiunga mkono Simba na kuishangilia Simba kwa nguvu zote inapocheza na timu za nje. Mtu yeyote anaekereka na taasisi ya kitanzania kufanya vizuri kimataifa basi ajue ana matatizo na upendo you ya taifa lake na inapaswa kuomba kupatiwa msaada wa tiba ya mkanganyiko wa mawazo .

    ReplyDelete
  4. Semeni ili msivunjike moyo, lakini mamba si shuari na ngojeeni mjuwwe mutabakiliwa na wachezaji wangapi

    ReplyDelete
  5. tafuten kauli ya msemaji wenu mr manara wkt yanga inacheza na usm alger ndo mjue uzalendo mnaoulazmisha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic