March 17, 2019

KIUNGO myumbulifu wa Simba, Haruna Niyonzima amesema kuwa siri kubwa ya ushindi kwa timu yake ni ushirikiano mkubwa na nguvu ya mashabiki waliojitokeza jana Uwanja wa Taifa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Niyonzima amesema kuwa hakuna kitu kizuri kama kucheza nyumbani ukiwa na mtaji mkubwa wa mashabiki ambao wamejitoa hali ambayo inaongeza morali kwa wachezaji kiujumla.

"Haikuwa kazi rahisi kupenya ila kikubwa ni namna ambavyo mashabiki wamejitokeza kutupa sapoti ni jambo la furaha na fahari kwetu, mashabiki waendelee kuwa na moyo huo nasi tutawafurahisha kwa kufanya kazi na sio maneno," amesema Niyonzima.

Ushindi wa Simba jana wa mabao 2-1 umewapa nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali ya Afrika jambo ambalo lilikuwa likisubiriwa kwa hamu na mashabiki na wachezaji kiujumla.

2 COMMENTS:

  1. amefanya kazi kubwa sana kama kiungo mnyumbufu

    ReplyDelete
  2. Hongera Haruna. Unaanza kulinda heshima yako.Simba walikuamini sasa lipia fadhila.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic