March 12, 2019


Beki wa kulia wa klabu ya Simba, Zana Coulibaly amemtaja beki mwenziye, Serges Wawa kuwa alisaidia kumpa nguvu ya kuendelea kusalia Simba.

Zana alisajiliwa na wekundu hao wa Msimbazi kwa ajili ya kuja kuziba nafasi ya Shomari Kapombe ambaye aliumia na sasa anaendelea kupata matibabu.

Beki huyo kutoka Burkina Faso ameeleza Wawa amekuwa akimpa moyo mchezaji huyo siku zote tangu atue Msimbazi.

Amesema alikuwa anapatwa na wakati mgumu kipindi kiwango chake hakijakaa sawa lakini baadaye baada ya kuanza kurejea vema mashabiki walianza kumuelewa vizuri.

Kutokana na kuwa tegemo ndani ya kikosi cha Simba, Zana amefunguka kuwa alitiwa moyo zaidi na Wawa ambaye pia alimwambia wakati anarejea Tanzania tangu atoke Azam miaka kadhaa iliyopita alikuwa anasemwa lakini kwa sasa mambo yanaenda vizuri.

"Namshukuru Wawa kwa kunitia nguvu na moyo wakati nawasili Simba sababu nilikutana na wakati mgumu.

"Mashabiki walikuwa wakinizomea na kunitumia lawama lakini baada ya kurejea vema uwanjani sasa wananielewa."

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic