MENEJA mpya wa Real Madrid, Zinadine Zidane ameanza kwa ushindi baada ya kuongoza kikosi chake kushusha kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Celta kwenye mchezo wa La Liga uliopigwa Uwanja wa Santiago Bernabeu.
Mabao ya Madrid yalipachikwa na Isco dakika ya 62 pamoja na Gareth Bale dakika ya 77 kwenye mechi ya kwanza ya Zidane katika kiksoi hicho.
Zidane aliikacha Madrid miezi 10 iliyopita amerejeshwa tena na uongozi ili kuendeleza gurudumu baada ya kikosi kuwa na mwenendo mbovu.
0 COMMENTS:
Post a Comment