BAADA ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi kukamilika kwa timu zote 16 kukamilisha ratiba zao hatimaye timu nane zimetinga hatua ya robo fainali.
Timu hizo kwa sasa zinasubiri droo ichezwe ndipo zijue zitacheza na nani kwnye hatua hiyo kwa sasa ni hizi hapa zilizotinga nane bora:-
Kundi A
Esperance na Horoya
Kundi B
Waydad Cansablanca na Mamelod Sundown
Kundi C
TP Mazembe na St Constantine
Kundi D
Al Ahly na Simba
Wa kaskazini mwa Africa wameingiza timu Nne 4,Africa magharibi timu moja,Africa ya kati timu moja,Afica ya mashariki timu moja na Africa ya kusini timu moja.Utaona jinsi gani Simba ilivyoibeba Africa Mashariki na vile vile kwa jinsi gani warabu walivyo vizuri kisoka kulinganisha na kanda nyengine za Africa. Simba wamefanya jambo kubwa kwa watanzania hasa vijana ambao ni kundi kubwa la watu miongoni mwa watanzania. Simba wametoa funzo kubwa kwa vijana hao la kuwaaminisha kuwa watanzania tunaweza na kamwe tusikubali kuaminishwa kuwa hatuwezi hata kama kauli hiyo inatoka kwa mzazi wako wa kukuzaa. kinachotakikana ni kujituma kwa malengo tu. Moyo wa mapambano uliooneshwa kwa vitendo na watu wa Simba katika kutafuta ushindi licha ya kutopewa nafasi pamoja na vikwazo vingi wanavyopambana navyo kwenye ligi ya mabingwa Africa basi iwe chachu na kuziamsha sekta nyengine hata zile zilizo mbali na michezo kujitasmini upya katika kuliletea Taifa maendeleo. Simba hongereni sana.
ReplyDelete