UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, unapenda kukanusha vikali taarifa zinazoendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’, amepokea fedha kutoka kwa kiongozi mmoja wa Yanga.
Taarifa hiyo ya kutengenezwa inasambaa wakati ikiwa imebakia siku moja kabla ya Azam FC haijacheza na Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) unaotarajia kufanyika Uwanja wa Uhuru, kesho Jumatatu kuanzia saa 10.00 jioni.
Ujumbe huo unaeleza kuwa “Mchezaji wa Azam atumiwa milioni 3 na mjumbe wa Yanga.
Mchezaji wa Azam, Sure Boy, amekutwa na milioni 3 kutoka kwenye namba ya mmoja kati ya wajumbe wa kamati iliyoteuliwa ya muda ya Yanga, mjumbe huyo ambaye jina tunalo (tutalitoa mkihitaji) alituma pesa hizo juzi majira ya saa 3:52:23 kupitia kwa wakala mwenye jina la Thobias Kiwavi jijini Dar.
Ikumbukwe kuwa Yanga wana mechi na Azam siku ya Jumatatu,” ilinukuliwa kutoka chanzo cha Sports EM.
Azam FC tunaamini ya kuwa taarifa hizi ni uzushi mtupu na zinakuja ili kumwondoa mchezoni mchezaji wetu na kuwachanganya wachezaji wetu kuelekea mechi hiyo, hivyo tunawaomba mashabiki wetu mzipuuze.
“Uongozi wa Azam FC unapenda kuutahadharisha umma kuwa uzushi unaoendelea kwa mchezaji wetu, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, kuwa amepokea pesa Tsh 3,000,000 kutoka kwa mmoja wa viongozi wa Yanga unafaa kupuuzwa na kwamba una nia mbaya kwa mchezaji wetu,” uongozi wa Azam FC ukitolea ufafanuzi suala hilo.








ss hyo m 3 inatushnda kuwapa wachezaji hata posho Leo tumpe sure boy àaaaha jaman tuache kuhadaa watyu
ReplyDeleteHizo ni njama ili Azam ichanganyikiwe na kumfanya yanga ishinde kwasababu kushindwa yanga ni dharba
ReplyDeleteba kubwa Sana na July mnyama akizidi kupanda. Yanga imeingiwa na hofu kubwa Sana kwahivo wameona wafanye hivo ili iwasaidie
vyanga wapate
Wanajihadaa wenyewe na kujishusha hadhi yao waliyoiweka kwa zaidi ya miaka ya Uhuru wa Tanzania.
ReplyDeleteUshauri wangu kwa Azam, wasijaribu kumuweka benchi Sure Boy siku ya kesho. Kocha ampange tena kikosi cha kwanza ili waadhirike na porojo zao hawa vyura. Mpira unachezwa uwanjani, wao wanachezea fitina! na ndio maana wanazidi kufeli, wameshapoteza uelekeo hawa.
Wamezoea majungu. Kila kukicha wanakuja na jipya.Nani anakumbuka
ReplyDeletemechi ya Ruvu Shooting na Yanga?Kipa wa Shooting kafanyiwa madhambi refa kapeta Yanga wakafunga goli la 2 nani alilalamika usipokuwa Shhoting wenyewe?Kuna mwandishi aliandika?Wacheni majungu kila timu ishinde michezo yake hamna namna.
Kumbe wanajificha kivuli cha Simba sc kuwa wananunuwa mechi haya sasa nao hii vip wakubwa juweni lile unalomsema mwenzio nawe ipo siku utasemwa tu malipo mengine ni hapa duniani, jamani mpira huchezwa uwanjani na si kinywani.
ReplyDeleteYanga asijidanganye na ndoto za Abunuwasi kwamba atachukua ubingwa hata ashinde michezo yake yote sita iliyobaki hachukui ubingwa na asipoangalia hata nafasi ya pili hachukui.Kwa sasa Yanga amebaki kwenye udhaifu wa fitina tu kuwa Simba wananua mechi mara marefarii wanachukua rushwa.Natamani siku moja timu hizi zichezeshwe na marefarii wa kutoka nje ya Tanzania ndipo mbichi na mbivu zitajulikana.Yanga apigie mahesabu ya ubingwa wa Azam FA cup na huko ni hatihati.
ReplyDelete