April 20, 2019



NYOTA wa zama ni wa timu ya Taifa ya Senegal aliyewika pia alipokuwa na timu ya Liverpool, El Hadji Diof amesema kuwa kinachoiponza timu ya Taifa kushindwa kupata matokeo ni uchovu wa wachezaji wake kwa sasa.
Diouf, yupo Tanzania akiwa ni mmoja wa wafuatiliaji wa michuano hii ya vijana chini ya miaka 17 ambayo imeandaliwa kwa mara ya kwanza nchini hapa huku ikitumia viwanja vya Chamazi na uwanja wa Taifa.
Diouf amesema kuwa kinachoikwamisha Serengeti Boys kupata matokeo chanya kwenye mechi zake ni uchovu walioupata baada ya mchezo wao dhidi ya Nigeria.
"Niliwaona Serengeti Boys wakicheza kwa mara ya kwanza dhidi ya Nigeria, ulikuwa ni mchezo mzuri na walitumia nguvu nyingi kupambana hali ambayo iliwafanya wachoke sana.
"Hivyo ili warejee kwenye ubora wao ni lazima wapate muda mwingi wa kupumzika na kurejea kwenye ushindani kwani kila timu inapambana kutafuta matokeo kwa sasa," amesema Diouf.
Serengeti Boys kwenye kundi A wanashikilia mkia baada ya kucheza michezo miwili na yote wamefungwa, leo watamenyana na Angola mchezo wa mwisho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic