April 20, 2019


KUELEKEA mchezo wa ligi kuu kati ya Kagera Sugar na Simba utakaopigwa saa 10:00 Jioni na kurusha moja kwa moja na Azam TV, uwanja wa Kaitaba, makocha wa timu zote mbili wameonyeshana tambo zao kabla ya mchezo kuanza.

Mecky Maxime ambaye kwa leo ni mwenyeji wa mchezo amesema kuwa anatambua madhaifu ya Simba na ukali wao ulipo hivyo vijana wake wakifuata mbinu alizowapa itakuwa ni rahisi kumdhibiti mnyama.

"Natambua napambana na timu ya aina gani leo, kushinda kwao kuna leta maana halisi ya timu ilivyo na namna ambayo itanifanya nianze kuwapigia hesabu za kubeba ushindi ambao ninatarajia kupata leo, ushindani ni mkubwa nami nipo tayari," amesema.

Patrick Aussems, Kocha Mkuu wa Simba amesema anatambua umuhimu wa mchezo wa leo na amewaambia vijana wake wafanye kazi moja aliyowaagiza uwanjani kutafuta pointi tatu.

"Najua ni mchezo mgumu na wenye ushindani ukizingatia nimetoka kucheza michezo mingi hivi karibuni na migumu, ila kikubwa ni utulivu na kujituma nina amini kila kitu kitakuwa sawa," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic