April 20, 2019


MSHAMBULIAJI wa Simba, Mnyarwanda, Meddie Kagere, amewachimba mkwara wachezaji wote wanaowania ufungaji bora, akiwemo mshambuliaji wa Yanga, Haritier Makambo kwa kuwaambia kwamba amesharudi kwenye ligi, hivyo wana kazi kubwa ya kumzuia asifunge mabao ya kutosha.

Mshambuliaji huyo kwa sasa amefikisha mabao 16, sawa na Salim Aiyee wa Mwadui wakati Makambo akiwa na mabao 15 huku John Bocco wa Simba akiwa na mabao 11.

Kagere alisema kuwa kwa sasa akili yake yote ipo kwenye ligi baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo haoni kitakachomzuia kufunga mabao ya kutosha kuisaidia timu yake.

“Jukumu ambalo lipo mbele yetu kwa sasa ni kushinda mechi zote za ligi ambazo zipo mbele yetu kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu na hilo ndiyo jambo kubwa kwa sasa baada ya kutoka kwenye michuano ya kimataifa.

“Ushindani kwenye kufunga ni mkubwa lakini wajue kwamba nimerudi na kazi iliyopo mbele yangu ni kufunga mabao katika kila mchezo, najua wao wanapambana kufunga kuzisaidia timu zao kama ninavyofanya mimi, japokuwa malengo ya kuwa mfungaji bora pia yapo ndiyo maana napambana kuwazidi wao,” alisema Kagere.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic