April 25, 2019


Kocha Mwinyi Zahera amesema uamuzi wa wachezaji kugomea mazoezi sababu ya kutolipwa mishahara yao kwa zaidi ya miezi minne KIMEMKERA kwa kuwa wachezaji hawakumshirikksha.

Wachezaji wa Yanga leo wamefika mazoezini leo asubuhi Polisi barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, lakini hawakufanya mazoezi wakishinikiza kulipwa mishahara yao.

Kocha huyo amefunguka kuwa amechukizwa na kitendo hichi akieleza wachezaji wake walifanya bila kutoa taarifa.

Aidha amesema kwa wale ambao hawatafika kwenye mazoezi ya kesho atawafukuza moja kwa moja wakakae makwao sababu hawana nia ya kuichezea Yanga.

Una maoni yoyote juu ya maamuzi ya Zahera?




11 COMMENTS:

  1. Kwanini wagome sasa hivi sio huko nyuma? Ingawa ni haki yao kuna kitu nyuma ya pazia.....Nyumba ya Yanga isafishwe....lakini pia sportspesa kama wadhamini si wanatoa pesa ya mishahara? Hapa kuna mkakati wa hujuma na kumtafuta ubaya kocha....ili aondolewe. Pia uchaguzi wa viongozi unatumika kama hujuma kwenye timu....usafi unatakiwa....kuondoa "magugu maji na takataka na mamluki"...Timu ya Wananchi na Wawekezaji ni Wananchi...Daima Mbele Nyuma Mwiko.....Yanga itashinda na itasimama imara siku zote!

    ReplyDelete
  2. hapo kachemka 80million alizopewa kapeleka wapi au magazeti yamepamba

    ReplyDelete
  3. Sielewi...kopo linachangiwa kila mwezi....Mechi ya Simba mbali na washabiki wengi kuwa wa Simba iliingiza zaidi ya mil 200..Harambee Dodoma mil 500 pamoja na ahadi inakaribia bil 1 na Sport Pesa wanatoa hela...Tunajua faini za kuingilia mlango wa uchochoro ni mil 16 hivi?hela ya Yanga inaenda wapi.Watanzania sio wajinga tuache kuchezewa viini macho...Hivi timu kama Biashara na Ndanda zinamudu vipi pale Yanga inaposhindwa?Tunadanganywa tu.Usajili wa bil 1 ndio tunasikia.Wakati wachezaji wananyimwa mil 30000000 zao za usajili.Kakolanya ni shujaa pale alipojiweka pembeni.Zahera akacheze yeye basi na achukue hayo mamilioni

    ReplyDelete
  4. Na bado kuna zaidi ya mil 600 za CAF kwa kushiliki michuano mwaka jana

    ReplyDelete
  5. Azam ashinde na kisingizio kiwe kwakuwa walikuwa hawajafanya mazoezi kutokana na migomo

    ReplyDelete
  6. Bwana Tino umesahau km kuna gharama za uendeshaji hapo timu inasafiri kucheza mechi zake za mashindano,mishahara ya waajiriwa( wachezaji,benchi la ufundi , utalala n.k),maradhi,posho na chakula kwa wachezaji wanapokua safari . Pesa iyo bado ipo tu. Wanadai miezi 3 uko nyuma taasisi inaendeshwaje sasa?

    ReplyDelete
  7. Zahera ni pimbi kwani si juzi tumesikia amekabiziwa kitita kwa ajili ya usajili sasa yeye badala ya kuwalipa wanao cheza tayari anawataka wengine halafu wenye yanga wapo kimya hivi amewafanyaje huyu pimbi mpaka kila siku mambo hayaendi

    ReplyDelete
  8. Kwa nionavyo mimi mambo yetu haya ya kiswahili basi hata Mo wa Simba angepewa ile Simba bure basi ingekuwa kitu cha Manufaa. Vitu viwili vifanyike ili kuinusuru Yanga tena haraka. Yanga iwe chini ya mikono ya serikali ndani ya uangalizi wa takukuru mpaka uchaguzi upite. Mbili kama kweli Mengi alitaka kuekeza Yanga akawekewa zengwe kwanini wahusika wasimpekeze tena kuja kuikoa Yanga? Mengi mfanya biashara mzoefu,msomi na anaejua kumanage kitu kwa faida na kukua kwanini bado anaekewa zengwe kuekeza Yanga? Yanga wangekwenda tu kwa mengi na kupewa kishika uchumba ili kiwasaidie kutatua matatizo yanayoikabili timu hivi sasa huku wakiharakisha mchakato wa hisa kamili. Mbona kama kuna wanachama wa Yanga wanaichawiya timu yao wenyewe ibakie katika hali ile.

    ReplyDelete
  9. Muda mwingi Yanga wameutumia kuwa kwenye vyombo vya habari.....wakati Azam, Simba na timu nyingine muda wao mwingi wameuweka kwenye matayarisho na maandalizi ya mechi (kimwili na kisaikolojia).....sijui ni kwanini????Kocha Mwinyi Zahera wekeza muda wako kufundisha mpira....hiyo jumatatu sijui itakuwaje hapo jangwani baada ya mechi Azam vs Yanga?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic