April 25, 2019


KWA mara nyingine Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amerudia kauli yake ya tuhuma za rushwa na michezo michafu kwenye Ligi Kuu Bara,anadai kuna timu kubwa inacheza mechi za timu nyingine.

Kocha huyo amekuwa akidai kuwa kuna klabu moja tajiri inayohonga marefa na wachezaji wa timu pinzani kwenye mechi dhidi ya Yanga na timu zingine za Ligi Kuu.

Zahera amedai kuwa timu hiyo imekuwa ikitoa kiasi cha fedha kwa waamuzi na wachezaji katika mechi zinazoihusisha Yanga. Akaenda mbali zaidi kwa kutolea mfano mechi yao dhidi ya Singida, JKT Tanzania na Mtibwa Sugar ambazo zote zimechezwa ugenini.

Amedai hadharani kwenye nyakati tofauti tena mbele ya vyombo vya habari kwamba uongozi wa timu moja kubwa umekuwa ukiahidi wachezaji wa timu pinzani fedha ili washinde.

Anadai kwamba wamepewa ushahidi na wachezaji wa timu hizo ambao baadhi yao waliwahi kuichezea Yanga katika misimu ya hivi karibuni na wana mapenzi na Yanga.

Maoni yetu sisi ni kwamba tuhuma za Zahera ni nzito sana na hazipaswi kupuuzwa kwa maendeleo ya soka la Tanzania pamoja na kuhakikisha mambo yanakwenda kwa haki.

Rushwa ni kitu kibaya sana kama kikiruhusiwa kustawi kwenye soka letu haswa katika kipindi hiki ambacho klabu nyingi hazina fedha. Takukuru na TFF ni vyombo ambavyo vinapaswa kuyafanyia kazi kwa kina madai hayo ya Zahera na ikiwezekana hata yeye mwenyewe aitwe avisaidie vyombo husika kwa masilahi ya soka la Tanzania.

Siyo sahihi na wala haikubaliki kwenye soka klabu kuhonga waamuzi na wachezaji wa timu pinzani(kama ni kweli) ili timu nyingine ifungwe.

Hiyo ni rushwa mbaya kabisa ambayo kila mwanamichezo anapaswa kuipiga vita ndio maana tunasisitiza kwamba vyombo husika viongeze umakini na viingie kazini kufanya kazi yao kukomesha hayo. Kama ni kweli hali hiyo ikistawi itaua kabisa soka letu na kila mara tutakuwa tunapata wawakilishi feki kwavile ushindani hautakuwepo.

Tuache soka lichezwe na kila mtu mwenye uwezo ashinde kwa haki uwanjani bila matumizi ya rushwa au mambo mengine mbadala.

Hali ya kupenyeza rushwa kwa waamuzi kutazinyima haki timu zingine na kufanya ligi yetu kupoteza mvuto kwavile baadhi ya timu ndizo zitakuwa zinatamba tu na kufanya zinavyotaka haswa kwenye wakati huu ambao mashindano hayo hayana mdhamini mkuu.

Tunakemea kwa nguvu rushwa michezo kwani kama ilivyo kwenye maeneo yote ni adui wa haki.

Tunavisisitiza vyombo husika kwenye Ligi Kuu Bara pamoja na mamlaka za Serikali zitoe macho mawili kwenye Ligi yetu ili kuhakikisha madudu kama hayo yanatokomezwa.

Kila mmoja anapaswa kushinda au kushindwa kwa haki na si kwa shinikizo la mtu, kikundi au timu fulani yenye nguvu ya fedha.

Tanzania lazima tubadilishe fikra zetu na tucheze soka uwanjani. Madai ya Zahera yafanyiwe kazi kwa umakini yasipuuzwe au kuchukuliwa kama jambo jepesi.

Yafanyiwe kazi ili hata kama ni jambo la uongo jamii ijue kuliko kuliacha liendelee kueleweka hivyo linavyovumishwa sasa.

5 COMMENTS:

  1. TFF Ipo pale kupokea taarifa mbalimbali kutoka vilabu tofauti. Kama Yanga wana ushahidi wapeleke barua tff ili swala lao lishughulikiwe. Kama anaongea kwenye vyombo vya habari TFF haiwezi kufanyia kazi maswala ya magazetini. Swala la mchezaji wa Stand United mbona walipeleka barua kuwa siyo RAIA au swala la Gustapha mbona Walipeleka vielelezo TFF. Salehe mpira una kanuni sake kama unaonewa hasa kwa swala zito la rushwa unapeleka vielelezo then uone kama hayaja fuatiliwa.

    ReplyDelete
  2. Lakini nyie waandishi si mfikirie tu mnachoongea sana na Zahera, najiuliza hivi huyu zahera asingekuja TZ je ungeandika nn maana makocha wote wapo kimya wanapambana na hali zao, hivi kweli mechi alizozitaja huyo zahera kafungwa na kutoa droo lakini hawa wanaozungumzwa ni Simba sasa kiwango cha simba kwa wachezaji na viwango vya yanga kwa wachezaji wa ligi kuu si naona vinaendana tuu kama kuna aiyee kamzidi makambo bado tunajiuliza jamani, huyu jamaa hataki hata kufungwa sasa leo na hili kesho hili hv yeye ndo ndimbo? soka latanzania limekuwa soka letu Sasa hyo rushwa ndo imewafanaya hata serengeti wamefanya vibaya kweli jamani, mm naona zahera anatafuta kick. Anajua sasa hivi kila atakachozungumza atafanyiwa kazi tuu waandishi wengine wameshampiga chini sasa huyu saleh page nzima ni zahera mmmmmmmm

    ReplyDelete
  3. Ufanywe uchunguzi kwa anayoyasema Zahersa. Ikiwa kuna ukweli, basi hatuwa zichukuliwe na ikigundulika kuwa uwongo basi htauwa kali zichukuliwe dhidi ya wanaotumia hutuma za uwongo ambazo zinwavunjia heshima za waheshimiwa

    ReplyDelete
  4. Waandishi wapumabavu kuleta mada ya kishoga kama hii. Kwanini wasimshauri Zahera yeye mwenyewe binafsi kwenda TFF kutoa ushahidi wake kama ana uhakika na anachokisema. Timu tajiri gani inayohonga ili ishinde? Kama ni Simba kakutana nao na timu yake wakampiga pale Taifa. Wakaja ndugu zake wa Congo Vita club akawapa mbinu zote za Simba lakini wakapigwa. Kaja Mazembe hapa kaponea chupuchupu.wamekuja warabu wakaskazini na jeuri zao wamepigwa na Simba.kuna timu gani hasa Tanzania ya kuizuia Simba isipate ushindi kama kweli watadhamiria kushinda na kuondosha dharau? Zahera anachokifanya kutaka kuwaaminisha watu kwamba Yanga ikikosa ubingwa basi ni kwa ajili ya hujuma wakati wachezaji wenyewe wa Yanga wanafika hadi miezi mitatu hawajalipwa stahiki zao huku wakisikia michango inachangwa kwa ajili ya usajili mpya na si kwa ajili ya wachezaji wa sasa. Mchezaji gani mpumbavu atakae kuwa na moyo wa kuipigania timu katika hali kama hiyo? Zahera anaokota maneno ya kipumbavu kutoka kwa mashabiki wa Yanga wasiojielewa na kuifanya habari kupitia wanaojifayanya waandishi wa habari.Ila Simba imeamua kumpeleka Zahera mahakamani ili akathibitishe madai yake na wapo siriaz.

    ReplyDelete
  5. mwandishi mbona unakuwa kilaza namna hiyo hv kwel ukiangalia kikosi Cha yanga unahs nichakushinda mech zote za ligi hii! acheni kubwatuka. Simba kapta kweny kipnd kigum miaka Kama mitano hv Leo yanga hata mwaka haujaisha wanalalamika na kuyarudi waliokuwa wanayafanya kipndi wanapesa za manji kumgeuzia Simba achen wafe na bakuli kwanaza nawao TRA iwaangalie make hawatoi rist za efd.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic