May 4, 2019


MGOMBEA nafasi ya Ujumbe wa Yanga, Rodgers Gumbo amesema kama akifanikiwa kuchaguliwa kuiongoza klabu hiyo atahakikisha benchi la ufundi linaboreshwa ikiwemo kumuongezea cheo kocha mkuu Mwinyi Zahera.

Kauli hiyo aliitoa juzi ikiwa ni siku moja tangu azindue kampeni za uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Mei 5, mwaka huu.

Gumbo kaliambia gazeti hili kuwa upande wake ameridishwa na kiwango kikubwa cha ufundishaji ambacho amekionyesha Zahera, kimetosha kabisa kumpa umeneja wa timu.

Gumbo alisema kocha huyo amefanikisha timu iongoze Ligi Kuu Bara na kuifikisha kwenye hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho akiwa na wachezaji wa kawaida.

“Kama unavyofahamu tangu kuanza kwa msimu wa ligi, Yanga imekuwa ikijiongoza kimaskini bila ya kuwa na mfadhili, lakini tunashukuru timu imekuwa ikifanya vizuri.

“Timu imekuwa ikifanya vizuri kutokana na jitihada kubwa inayofanywa na kocha katika kutengeneza timu na wachezaji hao alionao na kufanikiwa kuongoza ligi na kuifikisha timu katika hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho.

“Ni matarajio kumuona Zahera akiifanyia mengi mazuri katika msimu ujao mara baada ya kupatiwa fedha za usajili na kusajili wachezaji yeye mwenyewe wale anaowahitaji,” alisema Gumbo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic