Mgombea nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amepanga kuanza na mambo makubwa matatu mara baada ya kufanikiwa kushinda katika nafasi hiyo.
Kauli hiyo, aliitoa jana kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi huo zilizofanyika jana kwenye Makao Makuu ya Klabu hiyo yaliyokuwepo mitaa ya Jangwani na Twiga, Dar.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mwakalebela alisema baada ya kuingia madarakani atatumia nafasi yake ya uongozi kwa ajili ya kuunda mfumo bora wa uwekezaji na uendeleshaji wa klabu hiyo kwa kuwashawishi wadhamini kuingia kuwekeza klabuni hapo.
Mwakalebela alisema, pia atawashawishi viongozi wenzake kujenga Uwanja wa Kaunda uliokuwepo Makao Makuu ya klabu hiyo utakaotumika kwa ajili ya mazoezi ili kuepuka gharama zinazotumika katika kukodisha uwanja wa mazoezi.
Aliongeza kuwa, kingine atakachokifanya ni kuliboresha benchi la ufundi lilikuwepo chini ya Mkongomani, Mwinyi Zahera huku wakifanya usajili wa kimataifa na kisasa kwa wachezaji wenye uwezo na uzoefu wa kucheza Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa.
“Nina malengo mengi niliyopanga kuyafanya kama nikichaguliwa kuiongoza Yanga, kati ya hayo ni kutengeneza mfumo thabiti wa kuwaunganisha wanachama, kuimarisha matawi na kuanzisha matawi mapya hapa nchini.
“Kuboresha miundombinu ya klabu, yakiwemo majengo na Uwanja wa Kaunda na kupanga kujenga mkubwa wa kisasa utakaokuwa na hosteli za wachezaji.
“Nitaiimarisha Yanga kiuchumi kwa kuanzisha vitega uchumi mbalimbali vya michezo na kuweka uthibiti. Kuwa na utawala bora na uwazi wa mapato na matumizi ya klabu.
“Pia, nitaimarisha soka la vijana na wasichana na kuwa na bora yenye wachezaji mahiri barani Afrika na kingine kikubwa ni kuendeleza mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeleshaji ili kuleta matokeo chanya na hilo.
"Tutaanza haraka mara baada ya mimi kuchaguliwa kwa kuitisha mkutano mkuu wa Yanga na kutoa mapendekezo kwa wanachama,” alisema Mwakalebela.
0 COMMENTS:
Post a Comment