May 20, 2019


Mshambuliaji wa klabu ya Biashara United ya Mara Tariq Seif Kiakala amefanikiwa kufunga magoli sita katika mechi nne za Ligi kuu Tanzania Bara zilizopita kwenye dimba la Karume. Musoma.

Tariq akiwa chini ya Kocha Amri Said 'Stam' amekuwa na makali ya aina yae akiwa ndani ya Karume Stadium.

Katika mchezo wa leo uliopigwa mjini Musoma, Tariq amefunga mabao mawili pekee dhidi ya Ruvu Shooting ambapo Biashara United imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1

Biashara inapambana kupata matokeo katika mechi zilizosalia ili kukwepa kushuka daraja iendelee kucheza ligi kuu bara msimu ujao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic