May 6, 2019


MENEJA wa Arsenal, Unai Emery amesema kuwa kwa sasa hesabu zao zinahamia kwenye Ligi ya Europa baada ya kupoteza matumaini kumaliza Ligi Kuu England akiwa kwenye nne bora baada ya sare ya jana dhidi ya Brighton.
Washika bunduki hao wameachwa kwa jumla ya pointi tatu na kikosi cha Tottenham ambao wapo nafasi ya nne wakiwa na mchezo mmoja wa kucheza ila watatakiwa washinde mabao nane kwenye mchezo huo kuishusha Tottenham.
"Tunajua hali inazidi kuwa ngumu kwetu kutokana na mambo yalivyo ila hesabu zetu ni kuona tunashinda Ligi ya Europa.
"Tuna nafasi huku kwenye Ligi ya Europa kufanya jambo nzuri na la muhimu kwa ajili ya timu hivyo lazima tupambane kupata matokeo," amesema Meneja huyo ambaye ameshinda taji la Ligi ya Europa mara tatu akiwa na Sevilla.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic