May 6, 2019


MOHAMED Salah na Robert Firmino washambuliaji wa Liverpool, kesho wataukosa mchezo wa pili wa nusu fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.
Salah alishindwa kumalizia mchezo wao dhidi ya Newcastle baada ya kugongana na mlinda mlango Martin Dubravka kwenye ushindi wa mabao 3-2.
Firmino aliukosa mchezo huo wa Ligi Kuu England na kushuhudia wenzake wakipambana kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya misuli.
Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa maumivu yatamuweka nje Salah watakapokuwa nyumbani, Anfield wakiwa na deni la mabao 3-0 waliyofungwa mchezo wa kwanza.
"Wawili kati ya washambuliaji wazuri nitawakosa usiku wa kesho na tunatakiwa kushinda mabao manne.
"Sio kazi nyepesi kupata matokeo kwenye mchezo huo ila ugumu huo utatufanya tupambane ndani ya dakika 90 kupata matokeo ili tusherehekee ushindi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya," amesema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic