May 4, 2019


Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kwa sasa Waamuzi wamekuwa wakiogopa kuwapa Simba penati pale zinapotokea Uwanjani.

Aussems ameeleza kuwa tangu wapewe pointi tatu walipocheza dhidi ya KMC imeonekana kama timu yake inatengenezewa mazingira ya kushinda.

Kauli ya Aussems imekuja kutokana na moja ya tukio la mchezaji Emmanuel Okwi kuchezewa rafu eneo la hatari mwa Mbeya City jana walipocheza mchezo wa Ligi Kuu, lakini Mwamuzi akapeta.

"Tangu tupewe penati mbili katika mchezo dhidi ya KMC inaonekana kuna maagizo yametolewa kuwa tusipewe penati tena.

"Marefa wanaogopa kutupa penati maana kuna penati halali ambazo hatupewi.

"Sijajua tatizo ni nini cha msingi tumeshinda tumepata pointi tatu ndiyo lilikuwa hitaji letu.

"Sasa tunajiandaa na mchezo ujao."

7 COMMENTS:

  1. duh anataka kuwa kama Zahera kulalamika

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sio kulalamika..ile ni penalty ya haki kabisa walionyimwa Simba...na chanzo ni malalamiko ya matopeni Fc aka Jangwani FC kuwa Simba wanabebwa.Keshaweka sumu sasa waamuzi wanaogopa toa penalty kuogopa kufungiwa!Kama wewe ni bingwa utakuwa bingwa tu!

      Delete
  2. Zahera analalamikia mambo ya kipumbavu na hata akiambiwa atoe ushahidi wa kile anachokilalamikia anabakia kubadilisha story. Kocha wa Simba analalamikia vitu hata sasa nenda kwenye marejeo ya match utashangaa kwanini Simba inaumizwa kiasi kile halafu bado makocha wa timu pinzani wanafikiri Simba kabebwa? Match kati ya Simba na JKT Tanzania pale Uhuru ukiangalia utaingia kichefuchefu jinsi refa alivyoshindwa kutoa foul za wazi walizokuwa wakifanyiwa wachezaji wa Simba.wahenga walisema huwezi kumnenepesha kondoo aliekonda kwa kumkondeha yule alienenepa kwani kwa kufanya hivyo basi hasara si kwa kondoo bali ni kwa mchungaji.TFF lazima watambue utofauti wa Simba na timu nyengine za ligi kuu si kwa utofauti wa pesa bali utofauti halisi wa viwango vya mpira. Na kama lengo kubwa ni kuiona Simba ikiwa na kiwango sawa na African Lyon basi hongereni sana TFF kwa jitihada zenu hizo. Inafahamika yakuwa Yanga wana watu wao ndani ya TFF ambao kwa namna yeyote ile wasingefurahia kuiona Simba ikishinda match zake. Yanga ndio walioanzisha kampeni ya Simba anapendelewa kwa lengo la kuhakikisha kuwa Simba haipati maamuzi ya haki uwanjani.Yanga haohao ndio waliokuwa wakiihujumu Simba kwenye match zake za kimataifa kwa kusambaza taarifa za uongo mitandaoni na kuziambia timu za kigeni kuwa Simba ilikuwa ikipulizia sumu kwenye vyumba vya kubadilishia nguo. Mwanzo walianza na kasumba yakuwa Simba itashitakiwa kwa ushirikina na kuziambia timu pinzani za Simba kuwa Simba inaroga na walivyoona hoja hiyo haina mshiko wakarukia hoja ya Simba itapokonywa points kwa kufanya fujo walivyoona hoja hiyo haina mshiko ndio wakamalizia hoja ya sumu vyumbani. Funzo hapa kwa TFF ni kwamba je yupo mwamuzi alieadhibiwa na CAF kwa kuipendelea Simba klabu bingwa Africa?Je yupo mchezaji wa Simba alipewa kadi nyekundu klabu bingwa Africa mpaka hatua waliofikia? Je ipo adhabu yeyote au onyo iliopewa timu ya Simba kwenye klabu bingwa Africa kwa kujaribu kupata matokeo au ushindi wa match kwa njia ya udanganyifu licha ya kukutana na ngumu kabisa barani Africa? Jibu ni kwamba Simba ni miongoni mwa timu yenye nidhamu si Tanzania bali Africa. Licha ya kufungwa goli tano lakini hukuwaona wachezaji wa Simba wakipanic na kuanza kucheza foul za kijinga.Tulikuwa tukilalamika kuwa timu zetu wachezaji wake hawakuwa na nidhamu sasa tumekuwa na Simba ambayo hakika benchi la ufundi la Simba linastahiki pongezi katika kusimamia nidhamu kwa wachezaji wake na wachezaji wa timu nyengine hapa nchini wanatakiwa kujifunza kwenye masuala ya nidhamu lakini badala yake jitihada kubwa zinafanyika kuiondosha taswira nzuri ya Simba kwa kuwa tu Yanga inalazimisha kutaka kuwa bingwa? Wale marefaree waliochezeha Simba vs Alahaly au Simba vs vita kama wangechezesha match ya JKT vs Simba basi kama idadi ya wachezaji JKT wangelioweza kubakia uwanjani sidhani kama wangebaki saba.Simba walifungwa na Kagera sugar kocha na Kagera sugar wakajisifu na kocha wa Simba akakubali kushindwa mwisho wa habari. Lakini kama Simba ndio wangekuwa wameshinda match ile basi hadi hii leo tungesikia Simba kabebwa? Ujinga uwe kwa mashabiki lakini uanapoona hata wasimamizi wakuu wa masuala ya mpira nchini wanazungumza lugha moja za kijinga na mashabiki kwa kweli inaogepesha sana kwa maendeleo ya soka nchini.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nakubaliana na wewe kabisa.Yanga wamekuwa wakiifanyia hujuma Simba hata kwenye mechi za kimataifa..Timu yao ikicheza kwa Mkapa hawaendi kwa wingi ili kusaidia kopo kujaa wapate riziki zaidi..Ikija Nkana FC na As Vita wanajaza uwanja utadhani mechi yao wanahusuka! Ni Nkana na AS Vita waliotangulia kuwafunga Simba na uwanja wa Taifa mara zote mbili ulisisimka utadhani Dar imejaa Wazambia na Wakongo. Mtu anajiuliza hivi wale mashabiki wametoka waapi?Kumbe ni wa jangwani.Sasa mbona hawana msisimko kama huo wa kujaza uwanja siku timu yao inacheza?
      Katika mechi ya Simba na JKT, tumeona penalt zaidi ya moja zikikataliwa kutolewa!Sio kwamba sasa imegeuka Yanga ambayo ni kawaida kwake kushinda 1-0 na 2-1 ni kwa sababu namna maamuzi yalivyo hivi sasa Simba inanyimwa nafasi za kufunga!tunaomba anachofanyiwa Simba sasa na iwe hivyo hivyo kwa Yanga pia!

      Delete
  3. Alilosema mi suala la msingi kwanu sote tumeshuhudia tokeo hilo na Kocha WA Simba hawezi kufananishwa hata kidogo na Zahera na hili ni lilalamiko lake la Kwanza kulisikis. Kosa la Ausems Jana Kwa nionavo Mie ni uchaguzi WA wachezaji Kama vile Mia yake ni kujaribu uwezo wa baadhi ya wachezaji badala ya kikosi cha Kasi na ikawa kila mmoja kivyake

    ReplyDelete
  4. Zuhura aka Zahera ni sawa na mwanamke mwenye mimba changa..kulalamikia kila kitu hata visivyo vya msingi!

    ReplyDelete
  5. Like goli walilofunga yanga na Azam wangefunga Simba kesho yake ungesikia refa kafungiwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic