May 7, 2019



BAO lililofungwa dakika ya 17 kwa Azam FC kupitia kwa Dany Lyanga akimalizia pasi ya Mudathir Yahya halikudumu mpaka mwisho wa mchezo kwani dakika ya 70 Stand United kupitia kwa Alfadhil Mussa ilisawizsha bao hilo na kufanya wote wagawane pointi moja moja.

Kwa matokeo hayo yanaifanya Azam FC kuendelea kuwa kwenye mwendelezo wa kusuasua baada ya kufungwa na Yanga bao 1-0 uwanja wa Uhuru wanazikosa pointi tatu nyingine safari hii wakiwa ugenini.

Azam wanabaki nafasi ya tatu wakiwa na pointi zao 67 huku hesabu zao za kutwaa ubingwa zikizidi kufifia kwa sasa wamebakiwa ni mcihezo minne kukamilisha ligi msimu huu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic