May 7, 2019


SELEMAN Matola kocha wa Lipuli amesema kuwa kilichompa ushinda jana ni kuzitambua mbinu za Yanga mapema na kuzuia njia zote za kuwapa ushindi mapema wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho.

Akizungumza na Saleh Jembe, Matola amesema kuwa, haikuwa rahisi kumaliza mchezo ndani ya dakika 45 ila mbinu za kocha Zahera alizitambua na kufanikiwa kuzizuia.

"Haikuwa rahisi ila ilikuwa ni lazima itokee, mpira ni mbinu na nilitambua nacheza na timu ya aina gani hivyo nikawapa majukumu wachezaji wote wamefuata na tumepata matokeo.

"Timu ya Yanga ni wazuri kwenye utumiaji wa mipira iliyokufa pamoja na mashambulizi ya kushtukiza, hilo nililitambua na nilijua mshambuliaji wao ni Makambo basi nikawaweka watu wa kazi wamefanya kazi yao," amesema Matola.

Lipuli itacheza fainali ya kombe la Shirikisho na Azam FC mchezo utakaopigwa mkoani Lindi.


4 COMMENTS:

  1. Replies
    1. TFF na Simba wamefanya nini??.

      Delete
    2. acha vijisababu!TFF na Simba hazihusiki hapo kabisa

      Delete
  2. Matola kocha mzuri ila basi mambo tu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic