May 2, 2019


MAHAMED Abdallah 'Bares' Kocha Mkuu wa JKT Tanzania amesema kuwa bao moja walilofungwa na Simba dakika za lala salama limewashtua hivyo wamejipanga kulipa kisasi mbele ya Ruvu Shooting kesho.

Bares ataingoza JKT Tanzania kuivaa Ruvu Shooting kesho Uwanja wa Mabatini akiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wake mbele ya Simba uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Akizungumza na Saleh Jembe, Bares amesema kuwa kushindwa kupata matokeo ni pigo kwao hivyo wanajipanga kulipa kisasi kwa michezo iliyobaki ikiwa ni pamoja na mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting.

"Tumepoteza mchezo wetu uliopita hivyo tuna kila sababu ya kutumia makosa tuliyoyafanya kuyadhibiti ili tupate matokeo mchezo wetu unaofuata dhidi ya Ruvu Shooting.

"Ushindani ni mkubwa na kila mmoja anahitaji matokeo hakuna namna lazima tupambane kwani ligi bado inaendelea na michezo ipo mikononi mwetu ya kushinda," amesema Bares.

JKT Tanzania imecheza michezo 33 ipo nafasi ya 13 imejikusanyia pointi zake 39 kibindoni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic