May 2, 2019



NYOTA wanne wa kikosi cha Simba kesho wataukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City utakaochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya majira ya saa 10:00.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa watawakosa wachezaji wao wanne kutokana na kutokuwa fiti kiafya.

"Tutamkosa John Bocco, ambaye aliumia kwenye mchezo wetu dhidi ya JKT Tanzania, alishindwa kumaliza dakika 90, Asante Kwasi aliumia kwenye mchezo wetu dhidi ya Biashara United, Pascal Wawa aliumia kwenye mchezo wetu dhidi ya TP Mazembe na Shomari Kapombe.

"Wachezaji wote kwa sasa wanaendelea vizuri, tayari Kapombe na Wawa wameanza mazoezi yao binafsi ya gym ili kujiweka fiti, mashabiki waendelee kutuombea dua tufanye vizuri," amesema Manara. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic