May 20, 2019

KOCHA Mkuu wa Biashara United, Amri Said amesema kuwa amejipanga leo kupata matokeo chanya mbele ya Ruvu Shooting mchezo utakaochezwa uwanja wa Karume, Mara.

Akizungumza na Saleh Jembe, Said amesema kuwa mchezo utakuwa mgumu na muhimu  kutokuna na kutokuwa na matokeo mazuri msimu mzima kwa kikosi chake.

"Najua kwa sasa timu inapitia changamoto kubwa ya kushindwa kupata matokeo ila hilo halinipi taabu kwa kuwa morali imerejea na kila mchezaji anahitaji matokeo.

"Tupo tayari kushinda na tutapambana, mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti tukiwa nyumbani," amesema Said.

Biashara United baada ya kucheza michezo 35 imekusanya pointi  40 ikiwa nafasi ya 18 huku Ruvu Shooting ana pointi 42 nafasi ya 16 baada ya kucheza michezo 36.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic