May 20, 2019

BAADA ya mchezo wa kwanza kupoteza mbele ya Mtibwa Sugar uwanja wa Manungu, kocha wa Azam FC, Idd Cheche amesema kuwa lazima walipe kisasi kwenye uwanja wa nyumbani.

Akizungumza na Saleh Jembe, Cheche amesema kuwa wanakumbuka walifungwa mabao 2-0 ugenini hivyo nao wamejipanga kupata pointi tatu uwanja wa nyumbani.

"Tulipoteza mchezo wa kwanza, hivyo benchi la ufundi limetulia na kufanyia kazi makosa ya mchezo uliopita, mipango ipo sawa tunaimani tutalipa kisasi mchezo wetu utakoachezwa uwanja wa nyumbani.

"Kupoteza kwetu mchezo wa kwanza kulikuwa na sababu za kiufundi hivyo tumepata majibu ya kiufundi tutazijibu kiufundi," amesema Cheche.

Kikosi cha Azam FC, kitaikaribisha Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa ligi, uwanja wa Azam Complex Mei 22 mwaka huu saa 2:00 usiku.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic