NAHODHA wa Simba, John Bocco amevunja rekodi yake ya kucheka na nyavu aliyoiweka msimu uliopita kwa kuweza kuifikia msimu huu huku bado wakiwa na mechi mkononi.
Bocco ambaye msimu uliopita wa mwaka 2017/18 alimaliza akiwa amefunga mabao 14 msimu huu wa mwaka 2018/19 ameivunja baada ya kufikisha idadi ya mabao 15 huku akiwa na michezo mingine minne.
Kwa sasa Simba imecheza michezo 34 ikiwa imebakiwa na michezo minne ili kumaliza mechi zake za msimu huu ambao una jumla ya mechi 38.
Bocco amesema kuwa msimu huu hana mpango wa kuishia kufunga mabao 14 pekee bali anataka afunge mengi zaidi ya msimu uliopita.
"Msimu huu nataka nifunge mabao mengi zaidi ya msimu uliopita kwa kuwa uwezo upo na nia ninayo hivyo kikubwa ni ushirikiano na juhudi katika kazi," amesema.
Simba imefunga jumla ya mabao 72 imejikusanyia pointi 85 zinazoifanya ijikite nafasi ya kwanza kwa sasa kwenye msimamo.
0 COMMENTS:
Post a Comment