BASI LA SWEET AFRICA LAPATA AJALI MLIMA KITONGA
BASI la abiria la kampuni ya Sweet Africa lililokuwa linatoka mkoani Njombe kuelekea Dar es Salaam, limepata ajali leo majira ya asubuhi maeneo ya mlima Kitonga mkoani Iringa.
Taarifa za awali zinasema hakuna vifo isipokuwa abiria kadhaa wamejeruhiwa na wamekimbizwa hospitalini kwa akiwemo dereva wa basi ambaye amevunjika miguu
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa, Juma Bwire, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akieleza chanzo cha ajali ni dereva kushindwa kulimudu basi hilo wakati anateremka mlimani, hivyo kupoteza mwelekeo kwa kuacha barabara.
0 COMMENTS:
Post a Comment