May 23, 2019


Bosi wa Bodi ya Ligi ya Ligi Kuu Bara, Boniface Wambura, amesema kuwa ni rasmi Simba wamekuwa mabingwa wa ligi msimu huu.

Wambura amesema hayo kufuatia ushindi wa Simba dhidi ya Singida United wa mabao 2-0 ilioupata juzi kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida.

Akizungumza kupitia radio EFM, Wambura ameeleza kuwa Simba wametwaa ubingwa kulingana na dhamira yao ilivyokuwa.

Ameeleza kwamba kwa namna ambavyo kikosi chao kilivyokuwa hakika wamestahili kwani walionesha nia ya kutwaa taj la ligi.

Simba imefanikiwa kutwaa kikombe hicho kwa msimu wa pili mfululizo na kuandika historia ya aina yake baada ya kuhaha kwa takribani miaka mitano misimu kadhaa hapo nyuma.

5 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic