May 5, 2019


Klabu ya Yanga imemchagua Dkt. Mshindo Msolla kuwa mwenyekiti wake huku Fredrick Mwakalebela akishinda katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti.

Katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Bwalo la Polisi Oysterbay Dar es salaam, Dkt. Msola amepata kura 1,276 akimshinda mpinzani wake Dkt. Jonas Tiboroha aliyepata kura 60.

Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Mwakalebela amepata kuara 1,206 akiwashinda Janneth Mbene aliyepata kura 61, Titus Osoro aliyepata kura 17, Yono Kevela aliyepata kura 31 na Chota Chota aliyepata kura 12.

Matokeo kamili yakiwemo ya nafasi za ujumbe wa kamati ya utendaji yatakujia hivi punde.

2 COMMENTS:

  1. Mikia fc mtapata sana tabu Safari hii na hao viongozi wenu wenye elimu za kuunga unga hao! Hiyo ndo yanga bhana Bigup Msolla na Mwakalebela.

    ReplyDelete
  2. Tunaingoja hiyo miujiza iliyoahidiwa na hayo mabilioni atayokabidhuwa Zahera ya kuijenga upya yanga na hao wachezaji wapya WA mabilioni Hizo zote ni mbio za watoto za sakafuni

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic