May 7, 2019


Kikosi cha timu ya Coastal Union ya Tanga kimepaki kwa muda maeneo ya Bagamoyo kabla wakati kikitoka Tanga kuelekea jijini Dar es Salaam.

Wagosi hao wa kaya wamepita maeneo hayo huku ikiwa haijajulikana sababu ni nini na kesho watakuwa na kibarua cha mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.

Wakati Coastal wakiweka kambi Bagamoyo, kikosi cha Simba kimezidi kujifua kuelekea mechi hiyo.

Simba wameendelea na mazoezi katika Uwanja wa Bocco Veterani kabla ya kukipiga na Coastal Union kesho majira ya saa 10 kamili jioni.

4 COMMENTS:

  1. Simba hakuna cha kudharau timu. Wachezaji lazima waelewe yakwamba vita bado mbichi.Tuliona jinsi mechi na JKT Tanzania ilivyokuwa ngumu na Simba na mwishowe wakaenda kufungwa kihovyo 4-0 na ndugu zao wa Ruvu shooting. Hii inamaana kila tumu inaikamia Simba kupitiliza maelezo na dhahiri kutakuwa na motisha fulani unatolewa kutoka upande fulani kwa hizi timu kutaka kuifunga Simba au kuizuia isichukue ubingwa. Mechi tano Dar licha ya kuwa na ratiba isio rafiki lakini lazima ziandaliwe mikakati maalum ya ushindi. Hakuna cha kuzembea sasa, na benchi la ufundi lazima liwe makini katika mipangalio yake ya ndani ya uwanja.Mechi na prison Simba ilipata goli la mapema ilikuwa vizuri lakini mara nyingi Simba imekuwa ikianza mechi zake taratibu kitu ambacho sio kawaida ya timu kubwa.Tumeziona timu kama Mazembe,Ahly,vita nakadhalika jinsi zinavyoanza mchezo kwa pressure ya mwana ukome ili kumchnganya mpinzani na wakati huohuo wachezaji wapo sharp katika kuzitumia nafasi za kufunga kwa haraka na dio maana timu zisiokuwa makini zinapokutana na vigogo hivi utasikia mtu kapigwa nne kabla hata kipindi cha kwanza hakijaisha yote ni mipango tu ya ushindi. Azam licha ya kucheza legelege siku ya Yanga lakini utaona siku ya Simba watakavyokaza,
    halikadhalika kwa kagera sugar ilisikika jinsi kocha wao akichonga baada ya kupata ushindi kule Kagera.Mtibwa siku zote sio timu nyepesi mara nyingi huwa na vijana wanaokuwa na uchu ya maendeleo zaidi kwa hivyo siku zote hucheza kwa bidii ili waonekane.Mwisho wa siku mechi hizi zote zilizosalia hazitakuwa rahisi kwa Simba ni vizuri kujipanga kikamilifu kwa yeyote atakae kuja mbele.

    ReplyDelete
  2. Simba chukueni ushauri wa wapenzi wenu. Tunataka muwe SERIOUS chezeni mpira wa ushindani wafungeni mapema tu msidharau mechi hata moja. Tunataka mechi zote tushinde. Mechi 5 zinazofuata tutangaze ubingwa. Bagamoyo Coastal Union wamepita njia. Kama bus lao lilisimama ni wazi walikuwa wanajisaidia. Waje tu wapigwe magoli tunataka pointi 3.

    ReplyDelete
  3. Wamekwenda Huko kupata chochote

    ReplyDelete
  4. Tunataka kikosi cha kazi na si kikosi cha kuwajaribu waliokuwa hawakupata fursa ya kucheza hapo mwanzo. Ni pona au kufa msifanye kamchezo mukajilaumu baadae

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic