May 7, 2019


MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Luis Suarez amesema kuwa hatashangilia leo endapo atafunga bao kwa mguu wake dhidi ya Liverpool mchezo wa hatua ya nusu fainali ya pili wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uwanja wa Anfield.
Suarez, aliondoka Liverpool mwaka 2014 baada ya kucheza misimu mitatu na nusu alifunga na alishangilia alipocheza na Liverpool uwanja wa Nou Camp walipoibuka na ushindi wa mabao 3-0.
Alipomaliza kufanya hivyo aliwaomba radhi mashabiki wa Liverpool na kusema kwamba anawaheshimu mashabiki wa timu hiyo.
"Nadhani watu wanajua kazi ambayo nilifanya hapa, nadhani watakuwa na shauku ya kujua nini nitafanya, ila nitakuwa kimya kwa muda na ninaamini wapo ambao watakuwa na furaha zaidi yangu.
"Kushangilia kwangu wiki iliyopita kwa wale ambao wanajua kuhusu mpira na wale ambao wanapenda wanajua umuhimu wa jambo hili, ninawaheshimu mashabiki wa Livepool, kwa sababu nilifunga na kushangilia nahitaji msamaha.
"Kwa sasa ipo wazi kama nitawafunga tena sitashangilia kwa namna yoyote ile bao langu," amesema.
Suarez amecheza michezo 133 alipokuwa Liverpool kwenye michezo aliyocheza ndani ya uwanja wa Anfield na alifunga jumla ya mabao 82.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic