May 1, 2019


Kiungo Mshambuliaji wa timu ya Simba, Hassan Dilunga, amewaomba radhi viongozi na mashabiki wa JKT Tanzania baada ya kuwafunga jana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 likifungwa na Dilunga mnamo dakika ya mwisho kabisa ya mchezo na kuifanya Simba ipate alama tatu muhimu.

Baada ya mchezo Dilunga aliibuka na kusema anawaomba radhi JKT kwani aliwahi kuichezea timu hiyo na aliondoka bila ugomvi.

Dilunga ameeleza kuwa kwa sasa wako kwenye harakati za kuchukua ubingwa wa pili mfululizo hivyo hakuwa na namna ya kufunga.

Bao hilo linakuwa ni la pili kwa Dilunga akiwa na Simba kwani ikumbukwe alifunga la kwanza katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa katika mchezo walioshinda 2-1.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic