May 21, 2019



UONGOZI wa Singida United umesema kuwa kuelekea kwenye mchezo wao wa ligi dhidi ya Simba utakaochezwa leo uwanja wa Namfua wachezaji wametengewa donge la milioni tatu na laki sita endapo watamchinja mnyama.

Singida United ipo chini ya mchezaji wa zamani  wa Simba Felix Minziro ikiwa nafasi ya tisa baada ya kucheza michezo 36 na ina pointi 45.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema mchezo wa leo ni zaidi ya fainali kutokana na umuhimu wa pointi tatu hasa wakiwa nyumbani.

"Simba ni timu bora tunaiheshimu, tumetenga donge nono kwa wachezaji endapo wakishinda itakuwa kiasi cha shilingi laki mbili kwa mchezaji na kuna uwezekano ikaongezeka kutokana na sapoti ambayo tunaipata kutoka kwa uongozi wa mkoa wa juu. 

"Mezani kuna kama milioni tatu na laki sita hivi ambazo ni bonasi tu kwa wachezaji kuelekea mchezo wetu dhidi ya Simba na tuna imani ya kubeba pointi tatu nyumbani," 

"Simba wanataka kutangaziwa ubingwa kwetu nasi tunasema hicho kitu kinatukera na hakikubaliki kabisa," amesema Katemana.



1 COMMENTS:

  1. Hizo milioni tatu na laki sita ni kwakila mchezaji su wagawane timu mzima?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic