May 18, 2019


UONGOZI wa Simba umesema kuwa hautawaacha wachezaji wake muhimu msimu ujao kwa kuwa tayari mazungumzo yameshaanza kufanyika ili kuongeza mkataba wao.

Wachezaji wa Simba ambao kwa sasa mikataba yao inakamalika msimu huu na wanatajwa kusepa moja kwa moja ni pamoja na Emmanuel Okwi mwenye mabao 15 ambaye anatajwa kwenda kujiunga na timu za Uarabuni pamoja na kiungo Jonas Mkude.

Habari za ndani ya Simba zimeeleza kuwa hakuna mchezaji muhimu ambaye ataondoka kwa sasa kwa kuwa mipango ni kusuka kikosi upya.

"Wachezaji ambao mikataba yao inakamilika lazima waongezewe mikataba kama mwalimu atawapendekeza hivyo hakuna mchezaji ambaye ataondoka kwa sasa ndani ya Simba, mipango Ipo vizuri na kila kitu kinakwenda kama ilivyopangwa.kilieleza chanzo.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic