May 18, 2019

UONGOZI wa Ndanda, umesema kuwa mchezo wao wa kesho dhidi ya Simba utakaochezwa uwanja wa Uhuru utakuwa mgumu ila wamejipanga kubeba pointi tatu mbele ya Simba.

Akizungumza na Saleh Jembe, katibu wa Ndanda, Seleman Kachele amesema kuwa kikosi kimetia kambi muda mrefu Dar es Salaam hivyo uhakika wa kupata pointi tatu ni mkubwa.

"Kama kambi tumeweka muda mrefu hivyo hali ya hewa tumeshaizoea na wachezaji wana morali ya kutafuta pointi tatu, kila mmoja anatambua umuhimu wa mchezo wetu.

"Sapoti ya mashabiki ambao tunaipata ni kubwa na tuna kila sababu za kuwashukuru, hivyo neno letu bora litakuwa ni ushindi wetu kesho uwanjani," amesema Kachele.

Ndanda ipo nafasi ya saba imecheza michezo 35 na imejikusanyia jumla ya pointi 47.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic